Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan na Amiri Jeshi Mkuu, leo Julai 25,2024 amewaongoza wannachi na Viongozi mbalimbli wa Serikali katika siku ya kumbukumbu ya mashujaa waliopigania uhuru wa Tanzania iliofanyika Mji wa serikali Mtumba Mkoani Dodoma.
Aidha Rais Samia ameweka mkuki na ngao kwenye mnara wa mashujaa uliopo mji huo wa serikali Mtumba ikiwa ni sehemu ya maadhimidho ya siku ya kuwakumbuka mashujaa hao.
Kwa upande wake Brigedia Jenerali mstaafu Simba Waziri Simba ambaye ni mwakilishi wa wapigania uhuru na aliyepigana Vita ya Kagera mnamo Mwaka 1978 hadi 79 ameeleza namna alivyotekeleza majukumu yake.
“Baada ya sisi kufika pale Uganda tulikuta Idd Amin Dadaa ameshaondoka na ndege ya Libya na kwenda kukaa huko baada ya hapo akakimbia tena na kwenda Saudi Arabia kutokana na jeshi la Tanzania lilivyokuwa imara na tayari kwaajili ya kupambana nae”, amesema.
Naye F4053 XJKT Koplo Arseno Mapii ambaye alishiriki katika mapigano ya vita ya kagera amesema kuwa anakumbuka ilikuwa Februari 3, mwaka 1979 wakati ardhi ya Tanzania ikiwa imekombolewa wakati wakidhani vita imeisha ndipo hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere alipotangaza kuwa “Uwezo tunao, nia tunayo na sababu tunayo” hivyo wakapambane Uganda.
Nao baadhi ya Wananchi wametoa maoni yao kuhusiana na siku ya Mashujaa ambapo wamewahimiza vijana kujitokeza kwa wingi kwenye siku kama hizo ili kuendelea kujifunza yale yaliyofanywa na mashujaa wa nchi.