Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Rais Samia amewataka machifu wote nchini kusimamia maadili kwa vijana

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mkuu wa Machifu Nchini Dkt. Samia Suluhu Hassan amezielekeza wizara zote kuongeza mashindano na midahalo inayohusu maadili ili kuwapa nafasi vijana kujadili na kuzungumzia suala la utamaduni wa mtanzania.

Rais Samia ameyasema hayo leo Ikulu Chamwino Jijini Dodoma wakati akizungumza na machifu wa tanzania tukio lililoenda sambamba na utolewaji wa tuzo kwa baadhi ya machifu walio tekeleza vyema majukumu yao katika maeneo wanayoyatumikia.

Aidha, Rais Samia amewaomba machifu hao kuhakikisha wanasimamia vyema usawa wa kijinsia, utu pamoja na kujenga uaminifu kwa wananchi ili waweze kuwa kimbilio katika utatuzi wa changamoto mbalimbali.

Naye Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Damas Ndumbaro amesema kwasasa wanaandaa muongozo wa kuwatambua machifu na viongozi wa kimila ili wawe na vigezo vya kiutambuzi.

Awali akitoa salamu kutoka kwa machifu hao, Chifu Nyamiloada wa Iii Aron Mikomangwa amesema kuwa wataendelea kushirikiana na serikali ili kuendeleza mila na tamaduni za kitanzania licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali zinazowakabili katika kutekeleza shughuli zao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *