Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Kasi ya ushughulikiaji wa malalamiko ya uvunjwaji wa haki za binadamu na misingi ya utawala bora yaelezwa kuongezeka nchini

Imeelezwa kuwa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kwasasa imeongeza kasi ya ushughulikiaji wa malalamiko ya uvunjwaji wa haki za binadamu na misingi ya utawala bora kutokana na upatikanaji wa rasilimali fedha kwaajili ya uchunguzi ambapo kuanzia januari 2023 hadi mei 2024 tume hiyo ilifanikiwa kupoea malalamiko mapya 135 na kushughulikia jumla ya malalamiko 1020 na kukamilisha uchunguzi wa malalamiko hayo 236 huku uchunguzi wa malalamiko 784 ukiendelea.

Hayo yamebainishwa Leo Jijini Dodoma na Mwenyekiti wa tume hiyo Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ripoti mbalimbali za chunguzi zilizofanywa na tume kwa mwaka wa 2023/24.

Sanjari na hayo Jaji Mstaafu Mwaimu amesema miongoni mwa chunguzi zilizofanyika ni tuhuma dhidi ya jeshi la polisi ambapo tume ilithibitisha kutozingatiwa kwa taratibu za kisheria za ukamataji na ushikiliwaji wa watuhumiwa katika mahabusu ya polisi.

Pamoja na hayo Jaji Mwaimu amesema tume itaendelea kufanya uchunguzi katika matukio yanayojitokeza na yenye viashiria vya uvunjifu wa amani nchini ili kuhakikisha vitendo hivyo vinakomeshwa mara moja katika jamii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *