Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Jimbo la Shinyanga latumia Jumla ya shilingi bilioni 5.7 kutengeneza miundombinu ya barabara

Katika kuendelea kupambana na tatizo la ubovu na uharibifu wa miundombinu ya barabara katika jimbo la Shinyanga, Serikali imetumia Jumla ya shilingi bilioni 5.7 kwa ajili ya kutengeneza miundo mbinu hiyo kwa kiwango cha moramu pamoja na kuweka mitaro na makalavati kwa kutumia fedha za tozo na mfuko wa jimbo.

Takwimu hizo zimetolewa na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Patrobas Katambi wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa ilani ya CCM katika jimbo hilo kwa kipindi cha miaka minne tangu aongoze jimbo hilo na kuanisha kuwa jumla ya shilingi bilioni 1.5 ni fedha za tozo na mfuko wa jimbo ni shilingi bilioni 2.5.

Akizungumza katika kikao hicho Meya wa Halimashuri ya Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko amesema mafaniko ya utekelezaji wa miradi hiyo ya barabara katika jimbo hilo, fedha kutoka serikali kuu pamoja na makusanyo ya mapato katika halimashuri ya manispaa ya shinyanga yameongezeka kutoka shilingi bilioni 2 za awali mpaka shilingi bilioni 6 za sasa ambazo zimewezesha miradi hiyo kufanikiwa.

Kwa mujibu wa takwimu za utekelezaji wa miradi ya maendeleo zilizotolewa na Mbunge huyo zimeanisha kuwa miradi mbalimbali imeshatekelezwa kwa mujibu wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya Mwaka 2020/2025 ambapo ameitaja miradi hiyo kuwa ni pamoja na elimu, afya barabara, maji masoko, umeme, kilimo na mifugo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *