Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Mama mmoja mkoani Geita ajifungua mapacha wanne (4) kwa mpigo

Mwanamke mmoja aliefahamika kwa jina la Elizabeth Vicent mwenye umri wa miaka 30 Mkazi wa eneo la Majengo Mapya Kata ya Nyankumbu Halmashauri ya Mji wa Geita Mkoani Geita amejifungua watoto mapacha wanne wa kike kwa wakati mmoja hali iliyopelekea watoto hao kuzaliwa wakiwa na uzito pungufu.

Akielezea namna alivyojifungua watoto hao mwanamke huyo amesema amekaa kipindi cha miaka 5 bila kupata ujauzito toka alipojifungua mtoto wake wa awali na baada ya kupata ujauzito wa hao mapacha alianza kuugua sana na alipoenda hospitali kwa ajili ya vipimo alibainika kuwa na watoto 4.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Geita Dr. Thomas Mafulu amesema mama huyo alijifungua watoto hao julai 3, 2024 katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita kwa njia ya upasuaji kutokana na muda wa mama huyo kujifungua kutokamilika kwa miezi 9 inayotakiwa na kuongeza kuwa kwa sasa watoto wanaendelea na matibabu zaidi kutokana na kuzaliwa na uzito huo pungufu.

Akizungumza kwa niaba ya familia hiyo Mafole Mgasa amesema kutokana na mama huyo kujifungua kwa upasuaji hali ya kiuchumi ya familia hiyo imezidi kuwa ngumu hivyo wanaiomba jamii na watanzania kwa ujumla kuwasaidia kwa chochote ili kumudu mahitaji ya watoto hao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *