Kutokana na ongezeko la watoto wa mitaani katika Jiji la Mwanza, wadau pamoja na mashirika mbalimbali wameomba kujitokeza ili kuwasaidia watoto hao kwani kwa kiasi kikubwa wamekua wakikutana changamoto mbalimbali ikiwemo kufanyiwa ukatili wa kijinsia pamoja na kujiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Taasisi ya Mtetezi wa Mama iliyopo Mkoani Mwanza Minael Mndeme ambapo amesema kwa sasa kumekua na kundi kubwa la watoto wa mitaani wengi wao wakiwa tayari wameshaanza kujihusisha na matumizi ya dawa za kulevya hivyo kwa kuliona hilo taasisi hiyo imepanga kuja na tukio maalumu la kuwakusanya watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu ili kuwapa Elimu ya kuwasaidia namna ya kujikwamua kutoka kwenye makundi hayo.
Nao baadhi ya watoto wanaoishi mtaani wamesema baadhi yao wamejikuta wakiwa katika kundi hilo kutokana ugumu wa maisha katika familia wanazotoka huku wengine wakitelekezwa na familia hivyo wanaiomba serikali kuwasaidia kuwapa malezi ili waishi vizuri kama wanavyoishi watoto wengine.