Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Aliyejenga Daraja Mbadala Apigwa Marufuku Kutoza Fedha Wananchi

Na William Bundala,Kahama

Mkuu wa wilaya ya Geita Hashim Komba amepiga marufuku wananchi kutozwa fedha ili kuvuka kwa kutumia daraja la muda kutoka Kijiji cha Nyakabale kuelekea Nyamatagata katika Kata ya Mgusu wilayani humo hali ambayo imekuwa ikileta changamoto kubwa kwa wananchi wa eneo hilo na kusababisha shughuli za kiuchumi kukwama.

DC Komba amepiga Marufuku hiyo leo Juni 21,2024 wakati wa ziara yake ya kukagua miradi na kusikiliza kero za wananchi katika kata hiyo mara baada ya kufika katika daraja hilo nakukuta ujenzi unasuasua huku wananchi wakitozwa pesa kuvuka daraja mbadala liliojengwa katika eneo hilo licha ya serikali kutoa pesa za kujenga daraja la mda ili wananchi waweze kupita wakati ujenzi wa daraja ukiendelea.

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo Mwakilishi wa Meneja wa TARURA wilaya ya Geita Simon Buganga amesema ujenzi wa daraja hilo ulianza Februari 29,2024 ukitarajiwa kukamilika Juni,2024 kwa gharama ya kiasi cha shilimingi Milioni 400 huku akisema kabla ya kuanza ujenzi wa daraja hilo wananchi walikua wanatozwa na mtu binafsi aliyejenga daraja la muda lakini baada ya kuanza ujenzi wamlipa fidia na kuondoka.

Mkandarasi anaetekeleza ujenzi wa daraja hilo kutoka kampuni ya YUNICON ya jijini Mwanza Thurston Mgeni amesema sababu kubwa zilizopelekea daraja hilo kushindwa kukamilika kwa wakati ni mvua kubwa zilizonyesha Machi na kusababisha ujenzi kukwama huku akiomba kuongezewa siku 60 nje ya muda wa awali ili kukamilisha ujenzi wa daraja hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *