Na Costantine James,Geita
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa imewataka wandishi wa habari kuzingatia maadili ya taaluma ya uandishi wa habari wakati wa uwasilishaji wa maudhui kwa jamii ili kuepusha taharuki inayoweza kujitokeza kutokana na waandishi wa habari kushindwa kuzingatia kanuni na sheria nakupelekea kutoa maudhui yasiyofaa kwa jamii.
Rai hiyo imetolewa leo(Juni 4,2024) na Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya ziwa Mhandisi Imelda Salum wakati akitoa mada katika semina ya siku moja kwa waandishi wa habari Mkoani iliyolenga kuwajengea uwezo kuhusiana na uwasilishaji wa maudhui mtandaoni ambapo amesema maudhui ama habari yoyote ikiwasilishwa mtandaoni bila kufuata sheria inaweza kuleta taharuki kutoakana maaudhui hayo kuwafikia watu wengi kwa muda mfupi.
Baadhi ya waandishi wa habari walioshiriki katika semina hiyo wameipongeza TCRA Kanda ya Ziwa kwa kutoa semina hiyo ambayo wameielezea kwamba itakuwa msaada mkubwa kwao kutokana na kuwakumbusha kanuni na taratibu za kuzingatia katika kuwasilisha maudhui hasusani Mitandaoni.