RAS CP. Hamduni Aomba Ushirikiano Wa Madiwani Katika Kuwahudumia Wanashinyanga

Na Eunice Kanumba

Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga CP. Salum Hamduni amejitambulisha katika Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga baada ya kupokea kijiti hicho toka kwa mtangulizi wake profesa Siza Tumbo aliyepangiwa majukumu mengine na raisi Samia Suluhu Hassan huku akiomba ushirikiano kwa madiwani hao katika kutekeleza majukumu yake.


CP. Hamduni ametekeleza jukumu hilo katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga ambapo pia ametumia nafasi hiyo kuwakumbusha Madiwani wa manispaa hiyo kutoa hamasa na elimu juu ya ushiriki wa wananchi katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ili wajitokeze kwa wingi kushiriki.


“Waheshimiwa Madiwani Manispaa ya Shinyanga pamoja na watumishi wenzangu, baada ya kujitambulisha rasmi kwenu sasa niwaombe ushirikiano wenu ili nami niweze kutekeleza vema wajibu na majukumu yangu na pia twende tukasaidie kutoa elimu na hamasa kwa wanachama na wananchi wetu ili waweze kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa tarehe 27 Novemba, 2024,” amesema CP. Hamduni.


Aidha CP Hamduni amewataka Madiwani hao kwenda kushirikiana na Kamati za Usalama katika maeneo yao hasa katika kipindi hiki cha kuelekea katika chaguzi ili kuzui vitendo viavyoweza kusababisha uvunjifu wa Amani katika maeneo yao.


Akizungumza kwa niaba ya Meya wa Halimashauri ya Manispaa ya Shinyanga Naibu Meya wa Manispaa hiyo Zamda Shabani amemuhakikishia ushirikiano wa kutosha RAS huyo katika kutekeleza majukumu mablimbali lengo likiwa ni kupeleka maendeleo na kuwatumikia wananchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *