Vita zinazoendelea ndani ya Vita ya Israel na Hamas

Imeandaliwa na Ibrahim Rojala ,Kwa Msaada wa Mtandao

“Hata mchanga ulio chini ya miguu yetu umeungua,haiwezi kuvumilika unapotembea, Mitaa imetapakaa vifusi na majengo yaliyobomolewa,nimeona waliojeruhiwa wakiwa wamelazwa chini na huduma muhimu na bidhaa hazipatikani,Hakuna umeme wala maji. Hakuna zahanati wala dawa, Visima vimeharibiwa, maduka madogo na makubwa yamebomolewa, na kuna uhaba wa chakula”maneno ya mmoja kati ya wahanga wa kile kinachoendelea kati ya kati ya Israel na Hamas katika Ukanda wa Gaza.

Mpaka sasa licha ya Vita ya Silaha Kati ya Israel na Hamas kuendelea Katika Ukanda wa Gaza,kuna vita mbalimbali zilizochochewa na uwepo wa mapigano hayo ambayo hivi sasa kitovu chake ni katika eneo la Rafah linalokadiriwa kuwa awali lilikuwa ni makazi ya zaidi ya watu milioni moja.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina limesema hadi sasa watu milioni moja wamefungasha virago na kuukimbia mji wa Rafah kusini mwa Gaza, huku kukiwa na ripoti mpya za mashambulizi ya usiku kuamkia jana katika maeneo ya kusini, kati na kaskazini yanayofanywa na vikosi vya Israel.

Katika tarifa yake iliyotolewa kupitia mtandao wa kijamii wa X UNRWA limesema mji wa Rafah kwenye mpaka wa kusini wa Gaza na Misri ulikuwa nyumbani kwa zaidi ya watu milioni moja waliokimbia makazi yao kwa karibu miezi nane ya mashambulizi ya kila siku ya jeshi la Israel, kujibu shambulio la kigaidi lililoongozwa na Hamas kusini mwa Israel tarehe 7 Oktoba mwaka jana.

Haya yamejiri siku tatu tangu Rais wa Marekani Joe Biden kuzindua pendekezo la usitishaji mapigano kwa kuzingatia usitishaji wa hatua kwa hatua kwa vita hiyo, pendekezo likiripotiwa kujumuisha

Kulingana na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina maelfu ya familia zimelazimika kutafuta makazi katika majengo yaliyoharibiwa vibaya huko Khan Younis jiji ambalo liko kaskazini mwa Rafah, na linalokadiriwa kuwa na watu wapatao milioni 1.7. 

Imeripotiwa kwamba makao yote 36 ya Kambi za Wakimbizi huko Rafah hivi sasa sasa yamebaki mtupu bila watu na Shirika hilo la Umoja wa Mataifa limeendelea kutoa misaada ya msingi ya kibinadamu licha ya hali mbayá inayozidi kuwa ngumu na limeongeza kuwa takriban wanawake na wasichana laki sita na Elfu tisini wanakosa vifaa vya msingi vya usafi wakati wa hedhi, faragha na maji ya kunywa.

Likiangazia mapambano ya kila siku yanayowakabili watu walio hatarini sana huko Gaza, Shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya uzazi UNFPA  linakadiria kwamba karibu wanawake 18,500 wajawazito wamelazimika kukimbia Rafah.

Hadi sasa ni zaidi ya watu elfu kumi wamebaki Rafah wakikabiliana na hali mbaya na upatikanaji wa huduma za afya na vifaa vya uzazi na Afya ya mama na mtoto iko hatarini Zaidi katik eneo hilo.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP limesema kwasasa kuna kiasi kidogo linachoweza kuwafanyia watu ambao bado wako Rafah, ambako barabara zisizo salama hazifikiki vizuri na mashirika mengine mengi ya kibinadamu yametawanywa na mirindimo ya risasi na mabomu.

Katika taarifa ya kutia hofu juu ya kuhama kutoka Rafah tangu kuongezeka kwa operesheni ya jeshi la Israeli Mkurugenzi mkuu wa WFP Matthew Hollingworth ameonya kwamba wasiwasi wa afya ya umma sasa umevuka viwango vya janga, wakati sauti za mashambulizi, harufu ni sehemu ya maisha ya kila siku, ni ya kutisha.

Ameongeza kuwa watu wamekimbilia maeneo ambayo maji safi, vifaa vya matibabu na usaidizi havitoshi, usambazaji wa chakula ni mdogo, na mawasiliano ya simu yamesitishwa,wakati huo huo  Shirika la Umoja wa Mataifa linalofanya uchunguzi kwa kutumia satelaiti limesema zaidi ya nusu ya miundombinu yote katika Ukanda wa Gaza imeharibiwa tangu kuanza mashambulio kwenye maeneo ya WaPalestina,uchunguzi wake ukigundua kuwa zaidi ya majengo 137,000 yameathirika huko Gaza.

Makadirio hayo yanatokana na picha za satelaiti zilizopigwa Mei zilizolingalinishwa na picha zilizopigwa mwaka mmoja kabla ya shambulizi la Hamas la Oktoba 7 nchini Israel aidha limesema picha zimeonyesha kuwa majimbo ya Deir Al-Balah katikati mwa Palestina na Gaza huko kaskazini ndiyo yalioathirika Zaidi likisisitiza kuwa matokeo hayo bado ni sehemu ya uchambuzi wa awali, ambao ulikuwa bado haujathibitishwa katika eneo la tukio.

Hata hivyo bado Israel inaendelea na mashambulizi yake huko Gaza, na kwa mujibu wa wizara ya afya ya Gaza, takriban watu 40 wameuawa katika muda wa saa 24 zilizopita,Waziri wa mambo ya nje wa Misri Sameh Shoukry amesema zoezi la usambazaji misaada Gaza halitoendelea tena hadi hapo Israel itaondoka kwenye kivuko cha mpakani cha Rafah na kurejesha udhibiti wake chini ya utawala wa viongozi wa Palestina.

Waziri Mkuu wa Israel hana dhamira ya kubadili chochote katika Msimamo wake, Jumatatu ya Juni 3, vyombo vya habari vya Israel vilimnukuu Benjamin Netanyahu akisema awamu ya kwanza ya mpango wa amani unaoungwa mkono na Marekani wa kuachiwa huru mateka unaweza kutekelezwa bila usitishwaji kamili wa mapigano.

Netanyahu aliongeza kwamba kipaumbele cha juu cha Israeli huko Gaza ni kulisambaratisha kundi la Hamas, Serikali ya Israel inahisi kuwa mpango wa amani wa Marekani haujakamilika na Waziri Mkuu huyo anakabiliwa na shinikizo kubwa kutoka kwa baadhi ya mawaziri wake ambao wanatishia kujiuzulu endapo mpango wa usitishwaji mapigano utatekelezwa. 

Wakati Wapalestina Wakikimbia Rafah,kuna wale waliojaribu kurudi katika kambi ya wakimbizi ya Jabalia kaskazini mwa Gaza baada ya kufika katka kambi hiyo macho yao yamepokelewa na matokeo ya kiwango kikubwa cha uharibifu ambao ni matokeo ya operesheni ya wiki tatu ya jeshi la Israel katika eneo hilo dhidi ya Hamas na makundi mengine yenye silaha ya Palestina.

Hii Leo Juni 4,2024 Jeshi la Israel linasema raia wake ambaye pia alikuwa raia wa Uingereza Nadav Popplewell na wengine watatu waliuawa wakiwa pamoja katika eneo la Khan Younis wakati wa operesheni ya Israel katika eneo hilo.

Kwa halisi halisi iliyopo hivi sasa ni kwamba licha ya Israel na Hamas kuendelea na mapambano yao katika ukanda wa Gaza kuna vita kadhaa zinazoendelea kwa wananchi,mashirika ya Kimataifa n ahata nchi za Mashariki ya kati kwa Ujumla.

Maelfu ya raia wa Palestina hivi sasa wakati wakikimbia mapigano,wanakabiliana na njaa,ukosefu wa makazi,nishati,maji huduma za Afya,majeraha yaliyotokana na vita na ukosekana kwa mahitaji muhimu ya afya kwa wanawake,wasichana na Watoto katika kipindi ambacho hawajui ni ipi hatma yao katika kile kinachoendelea ndani ya ardhi yao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *