
Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan amemteua Prof.Masoud Hadi Muruke kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Walimu,amemteua Ishmael Andulile Kasekwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kushika nafasi hiyo kwa kipindi cha pili.
Aidha Rais Dkt.Samia pia amemteua Balozi Maimuna Kibenga Tarishi kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela,Bw.Martin Emmanuel kilimba ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Biashara Tanzania(TCB).
