Wizara ya fedha ya Marekani meweka vikwazo kwa raia mmoja wa Russia, na kampuni tatu zenye makao yake Russia ambazo imesema zilikuwa zinajaribu kukwepa vikwazo vya Marekani katika mpango ambao unaweza kuwa umeondoa zaidi ya dola bilioni 1.5 za kampuni ya chuma ya mmiliki tajiri mkubwa wa Russia Oleg Deripaska.
Deripaska, mwenyewe aliwekwa chini ya vikwazo vya Marekani hapo Aprili 2018, aliingia katika biashara ya chuma wakati Umoja wa Sovieti ulipoanguka, na kupata utajiri kwa kununua hisa katika viwanda vya bati.
Oleg Deripaska,bilionea wa Urusi ambaye amewekewa Vikwazo na Wizara ya Fedha ya Marekani.
Forbes ili-orodhesha utajiri wake mwaka huu ni dola bilioni 2.8. Hazina ilisema kuwa Juni 2023 Deripaska alishirikiana na raia wa Russia, Dmitrii Beloglazov, mmiliki wa kampuni ya Obshchestvo S Ogranichennoi, inayotoa huduma za kifedha yenye makao yake Russia.