White House kutathmini hadhi ya muda na Vibali kwa Wahamiaji

Ikulu ya Marekani (White House) inatathmini njia za kutoa hadhi ya muda ya kisheria na vibali vya kufanya kazi kwa wahamiaji nchini Marekani wanaoishi kinyume cha sheria ambao wameoa na kuolewa na raia wa Marekani.

Wabunge Wademocratic na Mashirika ya utetezi wa haki za binadamu yamemshinikiza Rais Joe Biden kuchukua hatua za kuwalinda wahamiaji nchini Marekani kinyume cha sheria huku Biden akizingatia wakati huo huo hatua za kiutendaji kupunguza kuvuka mipaka kinyume cha sheria.

Uhamiaji umeibuka jambo la wasiwasi kwa wapiga kura, haswa miongoni mwa Warepublican kabla ya uchaguzi wa Novemba 5 unaotarajiwa  kuwashindanisha Joe Biden kutoka chama Cha Democratic  na mtangulizi wake wa Republican, Donald Trump.

Hayo yanajiri katika Kipindi ambacho Trump amesema sera za Biden zenye vizuizi kidogo zimesababisha kuongezeka kwa uhamiaji haramu katika taifa hilo.

 Ikulu ya White House katika miezi ya hivi karibuni imezingatia uwezekano wa hatua za kiutendaji kuzuia wahamiaji katika mpaka wa Marekani na Mexico ikiwa vivuko hivyo vitafikia kizingiti fulani, na hivyo kuzua ukosoaji kutoka kwa baadhi ya Wademokratic na mawakili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *