Raia wamepiga kura ya maoni kwenye hatua kadhaa za Kiusalama zinazopendekezwa na Kiongozi wa Nchi hiyo kama njia ya kukabiliana na Magenge ya Uhalifu yaliyosababisha wimbi kubwa la machafuko
Maswali mengi waliyoulizwa wapigakura yanalenga kuimarisha hatua za usalama ikiwemo kulitumia Jeshi kupambana na magenge hayo, na kuongeza muda wa vifungo kwa wanaopatikana na hatia ya ulanguzi wa dawa za Kulevya
Ecuador imetikiswa katika miaka ya hivi karibuni na wimbi la machafuko, kwa kiasi kikubwa yakitokea Nchi jirani ya Colombia, ambayo ni mzalishaji mkubwa zaidi Duniani wa Dawa ya Kulevya aina ya Cocaine
Mwaka 2023, kiwango cha mauaji kilifikia hadi vifo 40 kwa kila Watu 100,000 kufuatia hali kuwa hivyo Rais Daniel Noboa, ambaye aliingia madarakani mwezi Novemba, alikuwa amependekeza hatua kali zaidi za kukabiliana na uhalifu unaohusiana na magenge wakati nchi hiyo ikikabiliwa na ghasia zinazoongezeka ambazo zimeshuhudia mameya wawili wakiuawa katika muda wa wiki moja.