Vita ya ufungaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara, imezidi kuwa tamu kwa viungo washambuliaji kufuatia nyota wa Azam FC, Feisal Salum ‘Fei toto’ kujibu mapigo ya Stephane Aziz Ki.
Fei toto amejibu mapigo hayo baada ya kufunga goli la ushindi dhidi ya Ihefu ambalo limeifanya Azam kuendelea kujikita katika nafasi ya pili ya msimamo wa Ligi Kuu Bara wakiwa na pointi 54.
Bao hilo ambalo alifunga katika dakika ya 13 ni la 14 kwa Feisal ambaye jana, Jumamosi alishuhudia mshindani wake katika vita ya ufungaji Aziz Ki akipachika bao la 15 katika mchezo wa watani wa jadi ambao Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Simba kwenye uwanja wa Mkapa.
Contact Us
P. O. BOX 71, Shinyanga, Tanzania
+255 766 408 253
info@jambofm.co.tz