Iran kutolipiza Kisasi kwa Israel

Afisa wa ngazi ya juu wa Iran amesema kuwa nchi hiyo haina mpango wa kulipiza kisasi kwa kile kinachoelezwa na vyanzo vya habari kuwa shambulizi la Israel katika mji wa Isfahan usiku wa kuamkia jana.

Afisa huyo ambaye jina lake halikutajwa, amenukuliwa na shirika la habari la Reuters akisema kilichotekea ni hujuma za kujipenyeza kuliko kuwa mashambulizi kama ilivyoripotiwa na vyanzo vya kigeni. 

Nae Waziri wa mambo ya nje wa Iran Hossein Amirabdollahian akizungumza na wajumbe wa mataifa ya Kiislamu mjini New York, amesema mashambulizi yaliyofanywa na droni ndogo hayakusababisha uharibifu wowote. 

Israel haijatoa taarifa yoyote juu ya mashambulizi hayo inayoripotiwa kuyafanya, na mshirika wake mkuu Marekani imekataa kujihusisha. 

Waziri wa ulinzi wa Marekani Lloyd Austin amefanya mazunguzo na mwenzake wa Israel, lakini taarifa kutoka mazungumzo yao imesema kuwa wamejadili masuala ya kupunguza mivutano, bila kuitaja Iran.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *