Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Mafuriko Yaua 33, Morogoro na Pwani,1014 Wakiokolewa Rufiji

Watu 28 kutoka katika halmashauri nane Mkoani Morogoro wamepoteza maisha kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha katika mkoa huo zilizobomoa nyumba 1035, makazi 6874 yakizingirwa na maji,hekari 34970 za mazoa mbalimbali zikiharibiwa pamoja na kusababisha athari kwa mifugo 1466 ndani ya mkoa huo.


Msemaji mkuu wa Serikali Mobhare Matinyi amebainisha hayo April 12,2024 wakati akizungumza na waandishi wa jijini Dar es salaam na kubainisha kuwa Wizara ya nchi Ofisi ya Waziri Mkuu imefanikiwa kufanya tathimini, ukaguzi na muongozo wa kufanya ukarabati wa miundombinu iliyoharika ya barabara, madaraja umeme na maji pamoja na misaada ya chakula na huduma ya afya kwa wahanga wa maeneo hayo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa na Rais Dkt Samia.


Akizungumza kuahusiana na athari zilizosababishwa na mvua hizo kwa mkoa wa Pwani,Matinyi amesema watu watano wamefariki dunia,watano wamejuruhiwa zimeharibu miundombinu mbalimbali,kusomba kituo cha Afya cha kijiji Cha Muhoro,kuharibu makazi katika kipindi ambacho watu 1014 wameokolewa wilayani Rufiji.


Katika kushughulikia athari zilizosababishwa na mafuriko na kuzingatia maelekezo ya Mh.Rais timu ya Mawaziri akiwemo na manaibu waziri,makatibu wakuu pamoja na wataalamu ilifanya ziara katika maeneo yaliyoathirika katika siku za idi mosi na ili katika wilaya za Rufiji,Kibiti na Kilombero zikiongozwa na Waziri Jenista Mhagama ambapo pamoja na kutoa salamu za pole za Mhe Rais Samia walifanya tahmmini na ukaguzi pamoja na kutoa miongozo ya namna ya kukarabati miundombinu iliyoharibiwa pamoja na kutoa maelekezo ya namna ya utoaji wa misaada.


Mafuriko ya Pwani na Morogoro yana uhusiano Gani?
“Ifahamike kuwa kuna uhusiano kati ya bonde la Mto kilombero na mto Rufiji,maji yanayotoka kilombero yanachangia asilimia 62 ya mto Rufiji ambao unakusanya maji kutoka mikoa mingi hapa nchini ikiwemo pia mito ya Ruaha mkuu na Ruhegu unaotokea mkoani Lindi wakati Ruaha Mkuu unatokea Iringa ukiwa unaunganika na matawi mengine yanayotoka katika mikoa mingine”amesema Matinyi.

Kipi Kimesababisha Mafuriko Rufiji?

Shughuli za kibinadamu zinatajwa kuwa miongoni mwa sababu zilizosababisha mafuriko katika eneo hilo licha ya wananchi kupewa elimu,aidha bwawa la Nyerere ambalo awali kupitia katika mitandao ya kijamii baadhi ya watu walieleza kuwa huenda limechangia mafuriko hayo kupitia taarifa ya Msemaji mkuu wa serikali limeelezwa kwamba limesaidia kuchelewesha kutokea kwa mafuriko hayo pia lilisaidia kupatikana kwa taarifa za dalili za uwepo wa mafuriko kama zilivyotolewa na Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *