Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Zuchu awaponza walimu, Songwe

Kufuatia kipande cha video kinachosambaa Katika mitandao ya kijamii ikionyesha wanafunzi wakicheza wimbo wa msanii Zuchu
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imewavua vyeo walimu wakuu wawili wa Halmashauri ya Tunduma Mkoa wa Songwe kwa kosa la kuwachezesha wanufunzi wimbo huo isiyoendana na maudhui ya elimu kitendo ambacho ni kinyume na maadili ya utoaji elimu nchini.

Akitoa tamko hilo leo nje ya Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma Waziri wa Elimu ,Sayansi na Tekinolojia Prof.Adolf Mkenda amesema wametoa uamuzi huo mara baada ya kuthibitisha kilichokuwa kinatembea mitandaoni na kuwasiliana na mamlaka za usimamizi ubora wa Elimu huku akibainisha kwa kuwa maadili ya ufundishaji hayaruhusu ukiukwaji wa maadili na kusema kuwa shule ni sehemu ya kufundishia malezi yaliyo mema tu hivyo vitendo hivyo haviruhusiwi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *