Staa wa muziki kutoka Lebo ya WCB, Zuchu amethibitisha kuachana rasmi na mpenzi wake ambaye ni boss wake kwenye lebo hiyo mtu mzima Diamond Platnumz.
Zuchu amethibitisha kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram, ikiwa ni siku moja imepita tangu Diamond apost video akiwa na Zari nchini Afrika Kusini.
“HELO FAN-MILLY .I HAD TO POST THIS TO CLEAR MY CONSCIENCE.KUANZIA LEO HII MIMI NA NASIBU (DIAMOND) HATUKO PAMOJA .I KNOW THIS HAS BEEN OUR THING BUT AS HARD AS IT IS KUMUACHA MTU UNAEMPENDA HII NAOMBA MUNGU IWE YA MWISHO NA NIANZE MAISHA MAPYA.MAPENZI NI HESHIMA KWA BAHATI MBAYA SANA HIKO KIMEKOSEKANA KWETU . .AS FOR HIM BADO TUNA KAZI ZA PAMOJA I WISH HIM AND HIS FAMILY THE ABSOLUTE BEST .TUMEISHI VIZURI LAKINI NADHANI HII SIO RIZKI .MWAKA HUU NIMEJIFUNZA KUSEMA HAPANA KWA KILA KITU KISICHONIPA FURAHA AMA BAADA YA KUSEMA HAYA NAONA KABISA NAENDA KUANZA UKURASA MPYA WENYE MAISHA YALIYOJAA FURAHA ,UHURU NA AMANI . AS FOR NOW KAZI IENDELEE AND I AM SINGLE 🍻.
YOURS TRULY ZUCHU ❤️,” ameandika Zuchu ambaye usiku wa jana alikuwa na Diamond na alihudhuria harusi ya dadayake Diamond