Zuchu afungiwa na nyimbo zake zapigwa marufuku

Mwanamuziki na staa kutoka Kundi la WCB Zuhura Othaman Masoud maarufu kama Zuchu, amefungiwa miezi 6 kutojihusisha na sanaa ya Zanzibar na nyimbo zake kufungiwa kupigwa kwenye vituo vya Zanzibar.

katibu mendaji wa baraza la Sanaa, Sensa, Filamu na Utamaduni wa Zanzibar Mhe. Omar Abdalla Adam amesema baraza limemfungia kwa kipindi cha miezi sita kuanzia sasa.
“Baraza lina wajibu wa kusimamia mila, silka desturi na utamaduni wa Mzanzibari, kwa hiyo linatamka rasmi kumfungia msanii Zuhura Othman Soud
(Zuchu) kufanya shughuli yoyote ya sanaa kwa Zanzibar kwa kipindi cha muda wa miezi sita kuanzia leo Machi 5, 2024′

Amesema wanafanya hivyo kutokana na
tabia yake kuimba nyimbo ambazo hazina maadili, hazifuati misingi na hazina afya njema kwa jamii ya Wazanzibari.
Pia, amesema licha ya msanii huyo kutokuwa na usajili Zanzibar lakini
amekuwa akiendesha shughuli zake za sanaa bila kupata kibali.
Mbali na adhabu hiyo, pia msanii huyo ametakiwa kulipa faini ya Shilingi Milioni moja kwa Baraza la Sanaa na aandike barua ya kuomba radhi na kuthibitisha kwamba hatafanya kosa hilo ndani ya kipindi alichofungiwa.

Amesema iwapo akishindwa kufanya
hayo zuio lake litaendelea kwa muda usiojulikana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *