ZOEZI LA UKAGUZI MAGARI YA SHULE LAZINDULIWA BUKOBA

Na Clavery Christian – Kagera.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kagera kupitia Kikosi cha Usalama Barabarani, limezindua rasmi zoezi maalum la ukaguzi wa magari ya shule, ikiwa ni hatua ya kuhakikisha watoto wanasafiri kwa usalama wanapokwenda na kurudi kutoka shuleni.

Katika zoezi hilo, jumla ya magari 35 ya shule yalifanyiwa ukaguzi, ambapo magari 7 yalibainika kuwa katika hali mbovu na yasiyofaa kwa usafiri wa watoto ambapo jeshi la Polisi liliwaagiza wamiliki wa magari hayo kuyafanyia matengenezo na kuyarejesha kwa ukaguzi wa pili kabla ya kuruhusiwa tena kutoa huduma.

ACP Yusuph amesema kuwa zoezi hilo ni endelevu na linatekelezwa katika wilaya zote za Mkoa wa Kagera. Lengo kuu ni kulinda maisha ya wanafunzi na kuhakikisha wanasafiri katika magari salama, yenye viwango vinavyokubalika kisheria.

Kwa upande wake, SP Peter Mtali aliwataka wamiliki wa magari ya shule kutekeleza matakwa ya usalama kwa ufanisi, huku akitoa rai kwa wazazi kuwa makini katika kuchagua huduma za usafiri kwa watoto wao.

Zoezi hili limepokelewa kwa matumaini makubwa na wakazi wa Bukoba, hasa wazazi, wakiamini kuwa litasaidia kupunguza ajali na kulinda maisha ya watoto shuleni.  

Zoezi hilo lilizinduliwa katika Manispaa ya Bukoba na ACP Yusuph D. Yusuph, ambaye ni Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, akishirikiana na SP Peter Mtali, Mrakibu wa Trafiki Mkoa (RTO), pamoja na timu ya wakaguzi wa magari.

Katika zoezi hilo, jumla ya magari 35 ya shule yalifanyiwa ukaguzi, ambapo magari 7 yalibainika kuwa katika hali mbovu na yasiyofaa kwa usafiri wa watoto ambapo jeshi la Polisi liliwaagiza wamiliki wa magari hayo kuyafanyia matengenezo na kuyarejesha kwa ukaguzi wa pili kabla ya kuruhusiwa tena kutoa huduma.

ACP Yusuph amesema kuwa zoezi hilo ni endelevu na linatekelezwa katika wilaya zote za Mkoa wa Kagera. Lengo kuu ni kulinda maisha ya wanafunzi na kuhakikisha wanasafiri katika magari salama, yenye viwango vinavyokubalika kisheria.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *