Kocha wa zamani wa Real Madrid, Zinedine Zidane ‘Zizou’ amepiga chini ofa ya kuwa kocha mkuu wa Timu ya Taifa ya Algeria.
Hii inakuja baada ya Chama cha soka Algeria (FA) kumwekea ofa kamabe ambayo ingemfanya kuwa kocha anayelipwa ghali zaidi Afrika.
Zidane alitakiwa kwa ajili ya kuchukua mikoba ya Djamel Belmadi aliyejiuzulu baada ya Algeria kusukumizwa nje ya AFCON 2023 kwenye hatua ya makundi.