Zimbabwe sasa ruksa mashindano ya kimataifa

Shirikisho la soka la kimataifa (FIFA), limeifungulia Zimbabwe kifungo cha miezi 18, kutoshiriki mashindano ya kimataifa, ikiwa ni siku kadhaa kabla ya kufanyika kwa Droo ya michuano ya kufuzu kombe la Dunia mwaka 2026, kwa bara la Afrika.

Zimbabwe ilifungiwa na FIFA mwezi Februari mwaka 2022, kufuatia serikali ya taifa hilo kuingilia masuala ya soka baada ya Kamisheni ya michezo na Burudani nchini humo kuivunja kamati ya utendaji ya ZIFA mwezi Novemba mwaka 2021.

Huku sababu kuu ikiwa ni juu ya madai ya matumizi mabaya ya pesa ambazo serikali ya Zimbabwe ilitoa kwa shirikisho hilo, kwa ajili ya ushiriki wa Zimbabwe kwenye fainali za Afcon mwaka 2019.

Kwa sasa kamati ya muda imeteuliwa kuendesha shughuli zote za ZIFA hadi pale uchaguzi wa kupata uongozi mpya wa Shirikisho hilo utakapofanyika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *