Jeshi la zima moto na uokoaji Mkoa wa Geita limesema linachukizwa na vitendo vya wananchi kutumia vibaya namba ya kutoa taarifa ya majanga ya moto pamoja na matukio ya maokozi kutokana na baadhi ya wananchi kuitumia vibaya namba hiyo kwa kupiga na kutoa taarifa za uongo.
Hayo yamebainishwa na kamanda wa jeshi la zima moto na uokoaji Mkoa wa Geita, Mrakibu Hamis Dawa wakati akizungumza na Jambo FM na kuwataka wananchi kuacha mara moja tabia hiyo.
Katika hatua nyingine kamanda dawa amesema kuna baadhi ya wananchi wa mkoa huo wamekuwa wakichelewa kutoa taarifa za majanga ya moto mpaka pale moto unapowazidi ndipo wanatoa taarifa za tukio hali ambayo inasababisha jeshi hilo kufika eneo la tukio wakiwa wamechelewa.
Wakizungumza na Jambo FM baadhi ya wakazi wa mkoa wa Geita wamesema vitendo vinavyofanywa wa wananchi wa mkoa huo kupiga simu zima moto na kutoa taarifa za uongo sio vyema hivo wamewataka kuacha taiba hiyo kwani inawanyima fursa wale wenye uhitaji kutokana na kutoa taarifa nakukuta namaba inatumika kwa watu wasio sahihi.