PUTIN HATAKI VITA IISHE – ZELENSKY

Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky amemtuhumu Rais wa Urusi, Vladmir Putin kuwa ni kikwazo cha kutekeleza uridhiaji wa kusitisha vita kwa siku 30.

Zelensky kupitia ujumbe wake aliouandika kwenye mitandao ya kijamii,  alieleza kuwa ulimwengu haujasikia jibu lolote kutoka Urusi, kuhusiana na pendekezo la usitishaji vita.

Hata hivyo muda mfupi baadaye, Putin alisema anakubaliana na pendekezo la Marekani la kusitisha mapigano nchini Ukraine kwa siku 30, lakini akisisitiza umuhimu wa kufanyia kazi maelezo yaliyomo katika pendekezo hilo.

Baadaye, Rais Zelenskyy akajibu kwa kusema Putin ni mtu mwenye hila na kwamba Kiongozi huyo anaweza kuchelewesha au kujaribu kuvuruga makubaliano hayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *