Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Zanzibar Kuandaa Michuano Ya Kagame Cup 2024

Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) limeipa Zanzibar haki ya kuandaa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati CECAFA Senior Challenge Cup 2024 (Kagame Cup).

Michuano ya CECAFA Senior Challenge Cup inarejea baada ya mara ya mwisho kufanyika 2019 nchini Uganda.

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF) Suleiman Mahmoud Jabir amesema amefurahishwa na michuano ya Kombe la Chalenji kwa wakubwa kurejea. “Kwetu Kombe la Chalenji ya Wakubwa ni kama Kombe la Dunia na kuirejesha kutasaidia kuimarisha timu zetu hata kufuzu zaidi kwa AFCON,” aliongeza Jabir.

Zanzibar pia imepewa haki ya kuwa mwenyeji wa michuano ya CAF Africa Schools Football Championship CECAFA Zonal qualifiers.

Uganda imepewa haki ya kuandaa michuano ya kufuzu AFCON U-17 Boys CECAFA Zonal, huku Tanzania ikiwa mwenyeji wa kufuzu kwa AFCON U-20 CECAFA Zonal.

Ethiopia imetunukiwa kuwa mwenyeji wa mechi za kufuzu za CAF Women Champions League CECAFA, na CECAFA Girls U-20 Championship.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *