
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameihakikishia Marekani kuwa Zanzibar itaendesha Uchaguzi Mkuu kwa Amani kwa ajili ya Maendeleo na maanufaa ya Nchi na Wananchi.
Rais Dkt, Mwinyi ameyasema hayo alipozungumza na Kaimu Balozi wa Marekani Tanzania Andrew Lentz aliefika Ikulu Zanzibar Kujitambulisha tarehe 15 Aprili 2025.

Aidha Rais Dkt, Mwinyi amemuelezea Balozi Huyo kuwa Serikali inathamini kuwepo kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (GNU) kwani imeleta Umoja ,Amani na Mshikamano wa Wananchi wa Itikadi Tofauti za Kisiasa na kuifanya Nchi kupiga Maendeleo katika Nyanja Tofauti.

Halikadhalika Rais Dkt,Mwinyi ameeleza kuwa Miaka Mitano sasa Nchi imebakia katika Amani Jambo ambalo Serikali inaendelea kuchukua kila juhudi Kuhakikisha Amani hiyo inakuwa ya Kudumu wakati wa Uchaguzi na Baada ya Uchaguzi.

Kwa upande mwingine Rais Dkt,Mwinyi amesema Zanzibar bado inahitaji Kusaidiwa zaidi hasa katika kuimarisha Uwekezaji katika Sekta za Kipaumbele za Uchumi wa Buluu na Utalii kwa Misaada ya Kifedha , Kujenga Uwezo wa Kitaaluma kwa Watendaji na Mafunzo.

Naye Kaimu Balozi Andrew Lentz ameihakikishia Zanzibar kuwa Nchi Hiyo itaendeleza Ushirikiano na Zanzibar Uliopo Kwa Miaka mingi katika Kuendeleza Miradi mbalimbali ya Maendeleo katika Sekta za Elimu , Afya na Utalii.

Akizungumzia Masuala ya kisiasa ameishauri kuzingatiwa kwa fursa za Mazungumzo na majadiliano Ili kuyapatia Ufumbuzi Masuala ya Kisiasa kwa Amani na kufanya Uchaguzi wa Amani.