Zana Duni zinavyatumika kuokoa Watu 2000 Waliofukiwa na Tope

Zaidi ya saa 72 baada ya maporoko ya tope kuimkumba nchi ya Papua New Guinea, wakazi bado wanatumia makoleo, vipande vya mbao na mikono kujaribu kufukua vifusi ili kuwafikia manusura kutokana na vifaa vizito na misaada kuchelewa kufika kutokana na umbali wa eneo la tukio huku vita vya kikabila vikiwalazimu wafanyakazi wa misaada kusafiri kwa misafara iliyosindikizwa na wanajeshi na kurejea katika mji mkuu wa mkoa, takriban kilomita 60 (maili 37) usiku.

Serikali ya Papua New Guinea imesema zaidi ya watu 2000 wamefukiwa na maporomoko ya matope yalioharibu kijiji kizima, na kuomba msaada wa kimataifa katika juhudi zake za uokozi na sehemu kubwa ya kijiji cha Yambali kilichoko mkoa wa Enga ilifunikwa baada ya kuporomoka kwa mlima Mungalo majira ya asubuhi siku ya Ijumaa ya Mei 24 na kusomba nyumba kadha na watu waliokuwa wamelala ndani ya yake.

Kituo cha kusimamia majanga cha Papua New Guinea kimesema katika barua yake kwa Umoja wa Mataifa kwamba maporomoko hayo ya matope yalifukia zaidi ya watu 2,000 wakiwa hai na kusababisha uharibifu mkubwa wa majengo, mashamba ya chakula na kuleta athari kubwa kwa uchumi wa taifa hilo.

Kituo hicho kimeiambia ofisi ya mratibu mkaazi wa Umoja wa Mataifa katika mji mkuu wa Port Moresby kwamba hali inasalia kuwa tete huku matope yakiendelea kuhama taratibu, na kusababisha hatari inayoendelea kwa timu za uokozi pamoja na manusura.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *