ZAIDI YA WATUMISHI 9,000 KUAJIRIWA KADA YA AFYA – KATIMBA

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Zainab Katimba amesema Serikali inatarajia kuajiri zaidi ya Watumishi 9,000 wa kada za Afya.

Katimba ameyasema hayo Bungeni jijini Dodoma na kuongeza kuwa waajiriwa hao watasambazwa katika maeneo mbalimbali na hasa yale yenye mahitaji makubwa.

Amesema, “mpaka wakati huu, kuna kibali kipya katika mwaka huu wa fedha cha zaidi ya Watumishi wa kada ya afya 9,000 ambacho nao wataajiriwa na kusambazwa katika maeneo mbalimbali na hasa yale yenye mahitaji makubwa.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *