ZAIDI YA WATU 160 WANAHOFIWA KUFARIKI BAADA YA NDEGE KUWAKA MOTO KOREA KUSINI…

Shirika la Zimamoto Korea Kusini limesema mpaka sasa takriban watu 167 wanahofiwa kufariki wakati ndege ya Jeju Air ilipotua kwa kuacha njia na kulipuka moto wakati ilipogonga ukuta wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Muan ulioponchini Korea Kusini siku ya Jumapili (Desemba 29).

Jeju Air ndege namba 7C2216, iliyowasili kutoka mji mkuu wa Thailand Bangkok ikiwa na abiria 175 na Wahudumu sita, ilikuwa ikijaribu kutua kwa muda mfupi kwenye uwanja wa ndege kusini mwa nchi hiyo, wizara ya uchukuzi ya Korea Kusini imesema.

Watu wawili ambao wote ni wahudumu wa ndege waliokolewa na maafisa wa Zimamoto na waliobaki wanahoofiwa kufariki dunia.

Ndege hiyo yenye injini mbili aina ya Boeing 737-800 ilionekana  kwenye vyombo vya habari vya ndani ikiteleza kwenye barabara ya ndege bila kifaa cha kutua kabla ya kugonga ukuta katika mlipuko wa miale ya moto na vifusi. Picha nyingine zilionyesha moshi na moto ukiteketeza sehemu za ndege hiyo.

Ndege hiyo aina ya Boeing 737-800, inayomilikiwa  na Jeju Air, ilitengenezwa mwaka 2009, Mkurugenzi Mtendaji wa Jeju Air, Kim E-bae ameomba radhi kwa ajali hiyo huku akiinama chini wakati akitoa taarifa kwenye televisheni.

Mkurugenzi amesema chanzo cha ajali hiyo bado hakijajulikana na kwamba ndege hiyo haina kumbukumbu za ajali na hakuna dalili za awali za hitilafu. Shirika la ndege litashirikiana na wachunguzi na kufanya kusaidia waliofiwa kuwa kipaumbele chake kikuu, Kim alisema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *