Zaidi ya watu 50 wameripotiwa kupata maambukizi ya ugonjwa wa macho mekundu (Red Eye) Jijini Dodoma ambapo idadi hiyo ya wagonjwa ni kuanzia mwezi Disemba mwaka jana.

Takwimu hizo ni kwa mujibu wa Mratibu wa huduma za macho Mkoa wa Dodoma Elizabeth Kiula wakati akizungumza na Jambo FM na kuongeza kuwa wagonjwa hao ni kutoka Wilaya mbili za Chamwino na Dodoma mjini.
Awali, akitoa taarifa kuhusiana na ugonjwa wa macho mekundu Mkurugenzi wa huduma za tiba Wizara ya Afya Prof. Pascal Lugajo kwaniaba ya mganga mkuu wa serikali anabainisha mikoa iliyobainika kuwa na visa vya ugonjwa huo. Mpaka sasa Mkoa wa Dar es Salaama pekee umeshuhudiwa kuwepo kwa wagonjwa 869.