Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Zaidi ya nyumba 100 hazionekani Hanang

Imeelezwa kuwa hadi sasa nyumba zaidi ya 100 zimepotea Kutokana na mafuriko yaliyotokea Hanang na kusababisha vifo vya watu 87 na majeruhi 137 kutokana na miamba laini ya milima ya Hanang kulowa na kutengeneza tope wakati wa mvua na hivyo kushuka na kuzibua banio la maji na kupelekea maafa.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Wa Idara Ya Habari Maelezo Na Msemaji Mkuu Wa Serikali, Mobhare Matinyi jijini Dodoma wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) uliofanyika Dodoma na kukutanisha viongozi wa vilabu 28 vya waandishi wa Habari nchini.

Matinyi Amesema timu ya wataalamu walichukua picha za sateliti kabla ya tukio kutokea na baada ya tukio hilo kutokea na baadaye wataalam wa Sensa ya Watu na Makazi wametoa matokeo ya sensa waliyoyafanya katika eneo hilo lililokumbwa na mafuriko na kubaini nyumba zaidi ya 100 hazipo yakiwemo maduka na soko.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *