Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Zaidi ya kilo 300 za bangi zateketezwa Mkoani Mara

Jeshi la Polisi Mkoani Mara imeteketeza zaidi ya kilo 300 za bangi na lita 300 za gongo zilizopatikana katika kijiji cha Ngasaro wilayani Rorya huku Jamii ikiomba serikali kuongeza juhudi katika mapambano dhidi ya dawa hizo.

Zoezi la uteketezwaji huo limefanywa na kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Ndugu Godfrey Mnzava ambapo amelipongeza Jeshi la polisi mkoa wa kipolisi Tarime-Rorya kwa kuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya.

Awali akitoa taarifa Mkuu wa Polisi,mkoa wa kipolisi Tarime-Rorya Festo Ukulule amesema wamefanikiwa kudhibiti kwa kiasi kikubwa matumizi ya dawa za kulevya kutokana na doria mbalimbali ambazo zimekuwa zikipangwa na kufanywa na Jeshi la Polisi.

Bi Mariam Otieno na Bertha Omolo wakaazi wa mkoa wa Mara wamesema matumizi ya bangi na mihadarati imechangia pakubwa kuharibu vijana mapambano hayo ya serikali dhidi ya dawa hizo yatachangia kwa kiasi kikubwa kusaidia vijana.

Mwenge wa uhuru bado upo mkoani Mara ukiendelea na mbizo zake kukagua,kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi,ambapo tayari umekabidhiwa na kuanza mbio zake katika halmashauri ya wilaya ya Musoma mkoani humo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *