Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela ametoa miezi miwili kwa mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Geita Zahara Michuzi kuhakikisha anakamilisha Ujenzi wa Zahanati tatu zilizotelekezwa kwa muda mrefu katika halmashauri hiyo ili kuwawezesha wananchi kupata huduma za kiafya kwa urahisi.
Shigela ametoa Maagizo hayo wakati alipokuwa anakagua ujenzi wa zahanati ya Bombambili, Mwatulole na Bwihugule ambazo zimetelekezwa kwa muda mrefu na kuagiza halmashauri ya mji wa Geita kuhakikisha kufikia Januari 15, 2024 zinaanza kutoa huduma.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita Zahara Michuzi ameahidi kutekeleza agizo hilo kwa muda waliopewa huku akimuomba Mkuu wa Mkoa kusadia kufikishwa kwa huduma ya maji na umeme katika zahanati hizo ili ujenzi unapokamilika zianze kutumika mara moja.