
Mtandao wa YouTube umetangaza mipango ya kuwaadhibu waandaaji na wapakiaji wa maudhui ya kupotosha au yasiyofanana kichwa cha habari na habari kwenye mtandao huo wenye lengo la kujiongezea Watazamaji au wafatiliaji.
Taarifa kutoka tovuti ya zee news ya India imesema Mchakato wa uondoaji utaanzia nchini India kisha kusambaa katika nchi nyingine mapema mwakani. YouTube itakuwa inaangalia picha na kichwa cha habari kilichoandikwa kama kinaendana na video iliyopo endapo ikiwa ni uongo basi video hiyo itaondolewa na inawezekana mhusika akafungiwa akaunti yake.
Mfano wa habari za namna hiyo ni zile zilizoandikwa misemo yenye kuvutia wasomaji na kuwashawishi wafungue kutazama video ilhali ni uongo, mfano wa habari ‘Rais ajiuzulu’ wakati video haielezi kujiuzulu kwa Rais.
Hivyo katika kukabiliana na hilo, mtandao wa YouTube umeanza kampeni ya kuondoa picha na habari za uongo zisizoendana na uhalisia wa video iliyotumwa hatua iliyotajwa kuondoa taharuki katika jamii.
YouTube inasema itapambana na uongo huo ambao inapotosha watazamaji, ikilenga hasa video zinazohusiana na habari muhimu za kisiasa au matukio makubwa ya dharua yanayotokea.