
Jeshi la Polisi Mkoani Kagera, linashikilia Gaudiozi Yepa (42), mfanyabiashara kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wa miaka 10.
Kamanda Polisi Mkoa wa Kagera Kamishina Msaidizi wa Polisi, Blasius Chatanda amesema mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo Januari 2, 2024 mtaa wa Bomani, uliopo Kata ya Kayanga Tarafa ya Bugene Wilayani Karagwe.
Amesema, Yepa alimrubuni mtoto huyo ambaye ni Mwanafunzi wa darasa la nne kwa kumwambia apande gari lake lenye namba za usajili T 639 BKP aina ya Peugeot ili ampeleke nyumbani kwao na baada ya mtoto huyo kupanda ndipo alimbaka kwa nguvu na kumsababishia maumivu mwilini.