YANGA YATOA ZAWADI YA CHRISTMAS DODOMA….

Klabu ya Dar Young African imefanikiwa kuifunga timu ya Dodoma Jiji kwa Magoli 4 kwa 0, mchezo uliochezwa leo Desemba 25, 2024 ndani ya uwanja wa Jamhuri Dodoma.

Magoli ya Yanga yamefungwa na Clement Mzize Dakika ya 18 na 37, Aziz KI aliyefunga dakika ya 28 na Prince Dube aliyefunga dakika ya 62. Kwa matokeo haya Yanga anaendelea kubaki nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi kuu akiwa na point 36 huku Simba akiwa na point 37.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *