Mabingwa wa Ligi kuu Tanzania bara, Yanga leo wameendeleza ubabe wao wa magoli katika mchezo wao wa Kimataifa ambapo umefaninyika leo huko dimba la Pele Kigali nchini Rwanda, dhidi ya Al-Merrikh.

Katika mchezo huo Yanga Sc imeweza kupata mabao miwili kutoka kwa Kenned Musonda pamoja na Clement Mzize ambapo mabao yote yamefungwa kipindi cha pili.