Yanga yamchinja mnyama goli 5 kwa Mkapa

Mchezo wa Kariakoo Derby umemalizika dakika 90 uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar Es Salaam kwa shangwe kubwa kwa Wananchi baada ya kuwachakaza Simba SC goli 5 – 1.

Kwa kipindi cha kwanza, Yanga SC walikuwa wamefunga goli 1 na Simba SC 1 ikiwa bao la Yanga SC limefungwa na Kennedy Musonda dakika ya 3 na la Simba SC akifunga Kibu Dennis dakika ya 8.

Kipindi cha pili, Yanga SC wamejizolea mabao mengi zaidi hadi kufikia 5 mwisho wa mchezo, kwa dakika ya 64 na 77 yalifungwa mabao mawili na Maxi Nzegeli na Aziz Ki akafunga bao moja kwa dakika ya 73, Pia kabla mchezo haujaisha dakika ya 87, Pacome Zouzoua akakamilisha mkono kwa kufunga goli la 5.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *