Yanga yaifuata Mamelodi

Kikosi cha Yanga SC kimeondoka nchini leo kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mamelodi Sundowns.

Yanga ambayo ilitoka suluhu (0-0) katika mchezo wa kwanza inahitaji ushindi au sare yoyote ya magoli kusonga mbele.

Endapo itafuzu, Yanga itaweka rekodi ya kufikia hatua hiyo kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *