YANGA YAIADHIBU GOLI 5 – 0 FOUNTAIN GATE….

Timu ya Dar Young Africans (Yanga) imeiadhibu Fountain Gate kwa kuifunga Goli 5-0 kwenye mchezo wa Ligi kuu uliyochezwa kwenye uwanja wa KMC Complex uliopo Mwenge jijini Dar es Salaam.

Goli za Yanga yamefungwa na Pacome Zouzoua ambaye amefunga mawili dakika ya 16 na dakika ya 45+1, bao la tatu limefungwa na Mudathir Yahya ‘Abas’ dakika ya 41 baada ya kupokea pasi kutoka kwa Clement Mzize ambaye kwenye mchezo huu ametoa pasi mbili zilizozaa mabao huku akifunga goli la tano, na goli la nne lilifungwa na mchezaji Jackson Shiga wa Fountain Gate baada ya kushindwa kuzuia mpira uliopigwa na Pacome Zouzoua.

Kwa matokea haya ya leo (Desemba 29) Yanga inafikisha pointi 39 katika michezo 15 ikiwa nyuma ya vinara wa Ligi kuu, Simba yenye pointi 40.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *