Klabu ya Yanga SC, imemtangaza rasmi Miguel Angel Gamondi, raia wa Argentina kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo akichukua nafasi ya Nasreddine Nabi, ambaye ameomba kutoongeza mkataba wake klabuni hapo.
Gamondi (59) ambaye ni raia wa Argentina, amewahi kuzinoa timu za Wydad Casablanca, Mamelodi Sundowns, USM Alger, CR Belouizdad, Esperance de Tunis pamoja na timu ya taifa ya Burkina Faso.