YANGA SC YAJIWEKA PABAYA CAFCL

Klabu ya Soka ya Yanga imekubali kichapo cha 1 – 0 katika mchezo wa kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, dhidi ya wenyeji wao, Silver Strikers

Mchezo huo wa mchezo wa kwanza wa Raundi ya Pili umefanyika katika uwanja wa Taifa wa Bingu uliopo Jijini Lilongwe Nchini Malawi hii leo Oktoba 18, 2025.

Silver Strikers walipata bao hilo la pekee kupitia kwa kiungo mshambuliaji Andulu Yosefe dakika ya 76.

Timu hizo zitacheza mchezo wa marudiano Oktoba 25 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa wa jijini Dar es Salaam na mshindi wa jumla atafuzu hatua ya makundi inayoshirikisha timu 16.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *