YANGA SC WALAANI TUKIO LA KUCHANIWA JEZI, KUFUKUZWA UWANJANI KWA MASHABIKI

Uongozi wa Young Africans Sports Club umesikitishwa na unalaani vitendo vya kupigwa, kuchaniwa jezi na kufukuzwa uwanjani kwa mashabiki wake katika mchezo wa Fainali wa Kombe la Shirikisho Afrika
uliochezwa Mei 25, 2025 katika uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Kupitia taarifa iliyotolewa kwa Umma hii leo na uongozi wa Klabu hiyo, umeeleza kuwa wao wanaamini kwenye uungwana katika mchezo wa soka, hivyo vitendo walivyofanyiwa mashabiki wao vinapaswa
kulaaniwa na Wadau wote wa soka nchini huku wakiziomba Mamlaka husika kuchukua hatua kali kwa wote waliohusika.

“Vile vile, Uongozi wa Young Africans Sports Club unatoa pole kwa mashabiki wote waliokumbwa na kadhia hiyo na unawataka mashabiki wote wa klabu hii, kuendeleza uungwana na kupinga chuki na uhasama
unaotaka kujengwa na makusudi baina ya mashabiki hapa nchini,” ilieleza taarifa hiyo.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *