Yanga Kujenga Uwanja Wao Jangwani

Rais wa Klabu ya Yanga, Injinia Hersi Said amethitibisha kuwa, GSM ameridhia kujenga uwanja wa klabu hiyo ndani ya Makao Makuu yao.

Injinia amesema hayo leo ambapo klabu ya Yanga inasherehekea miaka 89 tangu kuanzishwa, kwake.

“Mr. Ghalib Said Mohamed, GSM ameridhia kwa dhati kushiriki kwenye kufanikisha ujenzi wa uwanja wa kisasa wa Young African Sports Club, katika eneo la Makao Makuu ya klabu, Jangwani, Jijini Dar es Salaam’, amesema Injinia Said

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *