Meneja Habari na Mawasiliano wa Yanga SC, Ally Kamwe amesema si kweli kwamba Yanga wamekuwa wababe wa Simba kwa Kipindi kirefu kwa sababu ya udhaifu, bali wamekuwa wababe kwa kipichi hicho kutokana na ubora.
“Simba wanakuwa bora wanafanya maandalizi lakini wakifika uwanjani wanakutana na Yanga ambayo ni bora zaidi yao, ubora wa Yanga ndio unafanya uone Simba ni dhaifu, lakini wote huwa tunakuwa bora kabla ya dakika 90, baada ya dakika 90 ndio unaona udhaifu wa Simba.”

“Udhaifu wa Simba umetengenezwa na ubora wa Yanga, Simba ni bora lakini anapata udhaifu baada ya dakika 90 akicheza na Yanga,” alisema Kamwe.