Wote Waliokidhi Vigezo Kujiunga na Vyuo, Kidato cha Tano

Na Gideon Gregory,Dodoma

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mohamed Mchengerwa amesema Wanafunzi wote 188,787, waliokidhi vigezo wakiwemo wanafunzi wenye Mahitaji Maalum 812 wamechaguliwa na kupangiwa kujiunga na Kidato cha Tano katika shule mbalimbali nchini pamoja na vyuo vya kati katika fani mbalimbali.

Waziri Mchengerwa ameyasema hayo leo Mei 30,2024 Jijini Dodoma wakati akizungumza na Waandishi wa habari ambapo ameongeza kuwa Wanafunzi 131,986 wakiwemo wasichana 66,432 na wavulana 65,554 wenye sifa, wamechaguliwa kujiunga na Shule za Sekondari za Kidato cha Tano 622 zikiwemo Shule mpya 82 zinazoanza mwaka huu wa 2024.

“Ubora wa ufaulu kwa kuangalia madaraja, unaonesha kuwa Watahiniwa 197,426 (37.42%), walipata ufaulu wa Daraja la I – III, hali inayoonesha kuwa ufaulu wa watahiniwa wa mwaka 2023 umeongezeka kwa 0.47% ikilinganishwa na ufaulu wa Daraja la I – III wa watahiniwa 192,348 (36.95%) wa mwaka 2022”, amesema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *