Wizi vifaa vya SGR wadhibitiwa

Imeelezwa kuwa wizi wa vifaa vinavyotumika katika kutengeneza mradi mkubwa wa reli ya kisasa yakiwemo mafuta ya petrol,kwa sasa umedhibitiwa huku wananchi wa shinyanga wakitakiwa kutunza miundo mbinu hiyo ya reli kwani ina faida kwao likiwemo suala la upatikanaji wa ajira hususani katika kipande cha Tabora Isaka na Isaka Mwanza.

Taarifa hiyo imetolewa na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme huku akitoa wito kwa uongozi wa reli kuendelea kutoa ajira kwa wana Shinyanga ili wanufaika wa mradi huo wa reli ya kisasa wawe ni wazawa.

Kudhibitiwa kwa wizi katika mradi huo wa reli ya kisasa kumetokana na jitihada kubwa zinazofanywa na jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ambapo kamanda wa jeshi la polisi mkoani Shinyanga ACP Janeth Magomi amesema wameendelea kukamata vifaa mbalimbali ambavyo viliibiwa katika mradi huo yakiwemo mafuta ya Petrol na Simenti huku akiwataka wananchi kuendelea kutoa taarifa juu ya wale wote wanaohujumu miundo mbinu ya reli katika maeneo yao.

Mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa SGR kutoka Dar es laam hadi Mwanza una jumla ya kilomita 1219 na ulianzishwa April mwaka 2017 katika kipindI cha awamu ya tano chini ya hayati Dr John Magufuli na mradi huo umeshatoa ajira kwa watanzania 3526 kati ya hizo nafasi 2328 ni za ujuzi wa juu na nafasi 485 ni za ujuzi wa kati na ujuzi wa chini ni nafasi 713.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *