Wizara yakana kufuta bima ya watoto

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema mpango wa bima ya afya kwa watoto wanaojiunga kwa hiari (Toto Afya Kadi) haujafutwa, bali kilichobadilika ni utaratibu wa kuwasajili watoto.

Waziri Ummy ameeleza kuwa utaratibu wa sasa ni kwa watoto kusajiliwa shuleni kwa gharama ya shilingi 50,400 ili waingie wengi wasio wagonjwa na hivyo kuweza kuchangia wachache watakaougua.

Amesema Kwa sasa Toto Afya Kadi wamesajiliwa watoto laki 2 tu, na kuwahimiza wazazi na walezi kuwakatia bima ya afya watoto wao.

Aidha, Waziri amesema sera ya watoto wa umri chini ya miaka 5 au watu wasio na uwezo kupata msamaha bado haijafutwa, na kwamba hospitali zote za umma zinaendelea kuhudumia watoto wa umri chini ya miaka mitano kupitia utaratibu wa misamaha.

Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ilionesha kuwa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ulipata hasara TZS bilioni 204.65 mwaka 2021/22 kutokana na ongezeko la gharama za mafao ya matibabu na gharama za huduma kwa wanachama ambazo hazikulingana na mapato yaliyoongezeka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *