Wizara ya Nishati imeliomba Bunge kuidhinisha jumla ya Shilingi 2,246,745,445,000 kwa ajili ya matumizi ya wizara hiyo na taasisi zake, ambapo Shilingi 2,167,513,219,000 sawa na asilimia 95.7 ya bajeti yote ya wizara ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko ameyasema hayo hii leo Aprili 28, 2025 wakati akiwasilisha Hotuba ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati na Taasisi zake kwa mwaka 2025/2026 bungeni jijini Dodoma.

